AVP Fofana Amaral, nyota wetu wa Almasi na kiongozi mpendwa, anajitokeza wazi katika mahojiano haya kuhusu kujiamini ili kupata mafanikio katika uuzaji wa moja kwa moja. Soma ili kujua jinsi alivyotoka katika sehemu ya mazoea na alipojiunga na QNET kwa mara ya kwanza. AVP Fofana Amaral alianza kazi yake kama muuzaji wa moja kwa moja kwa kuchukua hatua ya imani, na kwa imani thabiti kwamba siku moja atafanikiwa. Pia anaelewa maana ya kuwa katika Klabu ya Mafanikio ya QNET, na jinsi ya kuwa Mfanisi wa QNET pia.
Ulijisikiaje mara ya kwanza ulipoitwa kwenye jukwaa kama Mshindi?
Ilikuwa hisia ya ajabu. Nilihisi kwamba nisingeweza kutembea hadi jukwaani, nilitaka kuruka! Mimi na timu yangu tuliitwa jukwaani kama Nyota wa Almasi. Nafasi ya Kupanda cheo QNET ulikua imejitokeza. Kwanza kabisa, sikuamini kwamba inawezekana kwangu. Mnamo 2012, sikuwa hata nikijaribu safu ya Klabu ya Waliofnaikiwa (Achivers). Hata hivyo, baada ya kuona watu wengi wakifanikisha hilo, nilijiamini zaidi. Siku moja, wakati Mpango mpya wa Fidia wa QNET ulikuwa umekamilika tu, niliamua kwenda kupanda cheo. Nadhani ni lazima viongozi wawe mfano kwa timu zao. Kwa hivyo, tuliposikia majina yetu hatimaye, ilikuwa wakati mzuri sana na ninaamini kila mtu anapaswa kupata hisia hiyo.
Tofauti na kupata kipato cha juu, ni sababu gani nyingine mtu anapaswa kujitahidi kuwa Mfanisi?
Naam, kwa mara ya kwanza, hunaendeshwa na mapato yenyewe – unaendeshwa na ukweli kwamba tunapaswa kufikia cheo kingine. Hii inasukuma watu kupata watu chini yao zaidi. Kipaumbele changu cha kwanza kilikuwa kujenga timu yangu ya mauzo. Kuwa sehemu ya kikundi, kuwa na mikutano ya kibiashara na safari za nje ya nchi pamoja, kukutana na Waanzilishi – hizi ndizo zilikuwa sababu za mimi na timu yangu kuwa na lengo la kuwa QNET Achievers; mapato yalikuwa ya pili.
Kuwa mwenye Mafanikio wa QNET ni jambo maalum ambalo IR wote wanahitaji kufanyia kazi. QNET inapokuchagua kwenda kwenye safari za motisha, ni fursa nzuri na uzoefu wa kipekee. Unaweza kukutana na Waanzilishi wetu wapendwa. Unaweza kusafiri nao na Achievers wakuu kote ulimwenguni. Huu ndio aina ya uzoefu ambao hautapata popote pengine. Ni kitu cha kipekee sana, na kila mtu anapaswa kufanya yote awezayo ili kwenda angalau mara moja katika maisha yake.
Tumeambiwa tangu mwanzo kwamba sekta ya kuuza moja kwa moja ni moja ambapo unaongoza kwa mfano. Kuchaguliwa miongoni mwa wasanii wengine bora na kualikwa na Waanzilishi wa QNET wenyewe ni thawabu kuu ambayo mtu anaweza kupokea katika ubia huu wa biashara. Tofauti na mapato ya juu, unahisi kweli kwamba umefanya jambo sahihi na kwamba wewe ni mshiriki wa kikundi cha watu bora.
Tuambie zaidi kuhusu Safari yako ya kwanza ya Motisha ya Klabu ya Achievers (Wafanikiwa)
Safari yangu ya kwanza ya Motisha ilikuwa London. Kwangu, ilikuwa safari yangu ya kwanza na Klabu ya Achievers na mara ya kwanza nilienda Ulaya! Ilikuwa ni kitu kipya kabisa, na cha ajabu. Nilifanya kila niwezalo kuchaguliwa kwa heshima hiyo. Nilipofika huko, nilikutana na Wafanisi wengine, Washirika wa V na, bila shaka, Waanzilishi. Tulienda kila mahali pamoja iwe tulikuwa tukinunua vitu, kutoka kwaajili ya chakula au hata kusafiri kwa meli. Tulitumia masaa mengi kuzungumza na kila mmoja wetu na kujifunza kutoka kwa kila mmoja. Ikiwa unafanya kazi kwa bidii na kutoa bora zaidi katika biashara yako, na katika kila kitu unachofanya, hukupa fursa hii ya mara moja katika maisha, basi endelea! Fanya kila uwezalo kuwa bora kwa sababu, siku moja, utaitwa kwa mkutano wa aina hii, na utajionea thamani ya safari hii.
Je, ni kumbukumbu gani unayopenda zaidi katika safari hiyo?
Nakumbuka katika safari ya saa mbili ya mto Thames, Dato Sri Vijay Eswaran alikuja pale nilipokuwa nimeketi na mke wangu nyuma, na kushiriki nasi maono yake. Ninapofikiria safari hii, hii ndiyo picha ya kwanza inayonijia akilini – Dato akija, ameketi karibu nasi, na kuzungumza kutoka moyoni mwake. Anatutakia sana tufanikiwe ili tufikie uwezo wetu kamili. Katika saa iliyofuata, alishiriki jinsi walivyoanzisha QNET, jinsi walivyojenga biashara, changamoto walizokabiliana nazo, na jinsi alivyotaka tupate mafanikio kama yeye.
Una ushauri gani kwa viongozi wanaotaka kujenga timu ya QNET Achievers (Wafanikiwa)?
Kwanza, viongozi wawe na haja ya kuunga mkono walio chini yao, na kupitisha taarifa zote muhimu kuwafanikisha timu zao. Mahitaji ya Kukuza Cheo cha QNET ni rahisi sana, lakini wakati mwingine hatupitishi habari na hatujazingatia vya kutosha. Katika QNET, tunakua ikiwa tunasaidia watu kukua. Tutafikia viwango vya juu zaidi ikiwa walio chini yetu watafikia viwango vya juu zaidi. Kadiri tunavyowaunga mkono, tutaenda mbali zaidi.
Iwapo ungeweza kushiriki kidokezo kimoja muhimu na wengine ili kufuzu kwa Klabu ya Mafanikio, itakuwa ni ushauri gani?
Fuata Mpango wa Fidia wa QNET na ufanye kazi kwa bidii. Unahitaji kujiwekea malengo na kuyafikia hatua kwa hatua, kutimiza mahitaji. Ukizingatia walio kuwa chni yako na kuwasaidia katika kupanda cheo, pia wewe utapanda . Saidia watu wengi kutengeneza pesa na sio wewe tu; fanya kazi kwa bidii na watu wako, na nina hakika utafikia viwango vya juu.
Je, unawahamasisha vipi wanachama wa timu yako kuwa Wafanisi?
Kulikuwa na nyakati nyingi ambapo nilihisi kwamba mambo hayasongi mbele; nyakati ambapo nilijitenga kwa sababu sikuweza kuona mwanga mwishoni mwa safari. Kisha, unajiuliza je, umefanya maamuzi sahihi na ikiwa mambo yatakuwa bora. Mambo haya hutokea, lakini unapaswa kujua kwamba kwa kila kitu unachotaka kufikia katika maisha, kuna gharama ya kulipa. Kadiri bei inavyopanda, ndivyo mambo utakayoyapata yanavyokuwa makubwa.
Unahitaji kujiamini na kuamini kuwa kile unachofanyia kazi kitatimia kwako. Usikate tamaa – sentensi hii ni rahisi sana, lakini yenye ukweli. Kwa hivyo, chochote kinachotokea, hata hali iwe ngumu, kaa chanya na ujiamini. Ongeza idadi ya mikutano na mawasilisho unayotoa, pata kile ambacho hufanyi vizuri na ujiboresha. Endelea kusonga, usiache kamwe, na utapata suluhisho njiani. Amini katika juhudi zako na, kabla ya kujua, mambo yataanza kuja pamoja.
Je, unakumbuka ulipofanya uamuzi wa kuendelea? Ni nani waliokusaidia katika nyakati hizo ngumu?
Nakumbuka sana wakati huo. Kuna sehemu tofauti za safari yangu ya QNET lakini mwanzo ulikuwa mwaka 2007-2008. Nilianza biashara mwaka huo na nilikumbana na changamoto nyingi. Nilikuwa India, nchi ya kigeni kwangu, na nilikuwa sina pesa wakati huo. Nilikuwa nimekopa pesa kutoka kwa watu na sikuweza kuzilipa bado, na walikua na pasipoti yangu. Ilikuwa ni hali ngumu sana. Huu ulikuwa wakati mkiongozi wangu uliniambia, “Fofana Amaral, hakuna kitu kizuri maishani kinachokuja rahisi – lazima kwanza ulipie. Kwa hivyo, ugumu wote unaokabili sasa, hii ndio bei unayolipa kwa kitu kizuri kitakachokuja.
Aliponiambia hivyo, nilianza kuona changamoto kama bei ya mafanikio. Na, badala ya kuwa chini, nilitiwa moyo zaidi! Wakati kiwango chako cha nishati kinashuka, unapoanza kuhisi mashaka na uwoga ndani yako, hiyo inamaanisha kuwa una changamoto inayolemea mgongo wako. Unapaswa kuitambua, kukabiliana nayo, kisha usonge mbele.
Ikiwa ungeweza kujisemea miaka 12-13 iliyopita ulipokuwa ukihangaika mwanzoni mwa safari yako, ungemwambia nini?
Ningemwambia, “Ikiwa uko katika biashara hii, ndoto zako zote tayari zimetimizwa.” Ukiwa QNET unaweza kufikia kila kitu unachotaka. Hakuna ndoto uliyonayo kwamba uuzaji wa moja kwa moja hauwezi kutimia. Itatoa hata mambo ambayo huwezi kuamini hivi sasa. Mambo ambayo nimepata kupitia biashara hii, sikuweza kufikiria kwamba siku moja ningekuwa nayo. Baada ya kufanya biashara hiyo kwa miaka miwili hadi mitatu, nilipoanza kupata pesa, nilinunua gari langu la kwanza na la pili. Siku moja, nilipokuwa nikiendesha gari huku na huko Abidjan nilifika mahali katika eneo la watu matajiri, ambapo matajiri wote walinunua nyumba karibu na bahari. Niliingia kwenye mgahawa wa hoteli niliouona ufukweni na kuketi kufanya kazi fulani. Nilimsubiri mhudumu aje, lakini nilichoona ni wanaume wawili waliokuwa wamekaa karibu na mazungumzo mazuri. Walinitazama na kusema, “Bwana, hapa si mahali pa umma, hii ni nyumba ya kibinafsi. Lakini unaweza kukaa kama ungependa, sio shida. Niliposikia hivyo niliwajibu, “Hii ni nyumba yenu?” Wakasema, “Ndiyo, tunamiliki mahali hapa.”
Sikuamini kwamba baadhi ya watu walikuwa na pesa nyingi hivyo za kumiliki nyumba kubwa, nzuri kama ile mbele ya fukwe ile. Eneo lote lilikuwa shamba la bei ghali, na ili mtu kutoka Abidjan awe na nyumba huko, lazima wawe wamepata mambo makubwa, kwa sababu wanakuja huko kwa ajili ya wikendi tu. Kwa hiyo, nikajiambia, “Ikiwa nitajisukuma na kufanya kazi kwa bidii, labda siku moja nitanunua sehemu ya shamba hapa.” Nilikuwa tayari kufanya biashara ya kuuza moja kwa moja kwa miaka mitatu wakati huo, mambo yalianza kufanikiwa, lakini sikuwahi kufikiria ningeweza kumiliki kitu kama hicho.
Leo, mimi ndiye mmiliki wa mojawapo ya sehemu bora zaidi katika eneo hilo. Ninamiliki zaidi ya ekari mbili. Baada ya miaka 13 katika biashara hii naweza kusema kweli kwamba kila kitu kinawezekana, hata mambo ambayo sikuweza kufikiria nyuma. Biashara hii ina uwezo wa kukupa kila kitu tunachotaka. Kwa hivyo, tunapaswa kujiamini, tunapaswa kuamini katika ndoto yetu, na tunapaswa kuamini katika QNET.
Mwanachama wa Klabu ya Wafanikiwa wa Nyota wa Almasi Mshiriki wa V Fofana Amaral ni mtu anayejua thamani ya kufanya kazi kwa bidii na kukuza timu nzuri. Ameweka wazi kwamba katika mapambano yetu ya kufikia mafanikio, mara nyingi tunasahau kwamba sio tu kuhusu sisi wenyewe. Kulingana na AVP Fofana Amaral, lazima pia tuwatunze watu wetu juu ya kujijali wenyewe. Tunamshukuru kwa mahojiano haya mazuri na ya kufahamu. Je, unachukua masomo gani kutoka kwa AVP Fofana Amaral? Tujulishe kwenye maoni.