FinGreen, programu ya elimu ya kifedha ya QNET, kampuni ya kimataifa ya ustawi na maisha inayolenga kuuza moja kwa moja, imefanikiwa kutoa mafunzo kwa takribani watu 700 wakiwemo wafanyabiashara wadogo, vijana na wanawake wanaoendesha biashara ndogo ndogo, mjini Accra, na pia katika mji mkuu wa kikanda wa Mkoa wa Volta, Ho.
FinGreen ilizinduliwa na QNET mwezi Oktoba kwa ushirikiano na kampuni kuu ya uhasibu ya Ghana ya JA Abrahams, kama programu ya bure ya kunufaisha jamii ambazo hazijafikiwa vizuri nchini Ghana, ambazo mara nyingi ziko hatarini kutapeliwa kifedha na kukopeshwa kwa ulaghai, kutokana na ujuzi mdogo wa kifedha. FinGreen inaangazia vijana, wanawake, na wamiliki wa biashara ndogo ndogo, ikiwapa zana zinazohitajika kwa maamuzi ya kifedha ya kibinafsi na ya kibiashara.
Tukio la uzinduzi wa FinGreen, lililofanyika Accra mnamo Oktoba 24, 2023, lilivutia safu ya kuvutia ya waliohudhuria, ikiwa ni pamoja na wataalam wa kifedha, viongozi wa sekta ya benki, maprofesa wa vyuo vikuu, maafisa wa serikali za mitaa, wanafunzi, na wafanyabiashara wa kike, pamoja na vyombo vya Habari muhimu. Mkutano huu uliangazia hitaji muhimu la ujuzi wa kifedha na ulionyesha mbinu ya kina ya FinGreen ya kushughulikia changamoto hizi.
Sauti kutoka Washiriki katika Mpango wa Fingreen
Bw.Lawrence Adjatey meneja wa mpango mdogo wa kuweka akiba na ukopeshaji fedha maarufu kwa jina la ‘Susu’, alisema amejifunza jinsi ya kusimamia vyema fedha za wachangiaji wa susu na kufanya maamuzi ya haraka na sahihi ya kifedha yatakayoboresha mpango huo.
Bi. Abass Bushira, kijana wa kike anayeongoza ubia wa kilimo alisema: “Mafunzo ya FinGreen ni kama kama yalitengenezwa kwaajili yangu. Mtaala ulijumuisha mada kama vile bajeti, mikakati ya uwekezaji, usimamizi wa madeni, benki, mipango ya kifedha na mengine. Haya ni maeneo ambayo yanafaa sana kwa biashara yangu na fedha zangu. Hakika nimejifunza mengi na niko katika harakati za kuboresha biashara yangu na maisha yangu.”
Kulingana na Robert Kwasi Asmah, kiwango cha 400 cha Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Kitaalamu, Accra, alijifunza jinsi ya kusimamia fedha zake vyema na jinsi ya kuchanganua mambo hatarishi yanayoathiri fedha zake. Aliongeza kuwa sasa yuko katika nafasi nzuri ya kuwashauri wengine jinsi ya kusimamia fedha zao za kibinafsi.
Mtaala wa FinGreen, ulioundwa kulingana na muktadha wa Ghana, umeundwa ili kufikiwa na kufaa, kuhakikisha washiriki wanaweza kutumia maarifa yao mapya kwa ufanisi. Mpango huu unawezeshwa kupitia ushirikiano wa kimkakati na J. A. Abrahams & Co, kampuni mashuhuri yenye umri wa miaka 65 yenye utaalam wa kina katika huduma za uhakikisho, uhasibu, kodi, na huduma za ushauri wa biashara. Awamu ya kwanza ilianza Oktoba na itaendelea hadi Desemba 2023.
FinGreen inawiana kikamilifu na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na Ajenda ya Addis Ababa, ikitambua kwamba kufikia ushirikishwaji wa kifedha ni sehemu muhimu ya maendeleo endelevu. Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2022 nchini Nigeria na Uturuki, FinGreen ya QNET imewawezesha takriban watu 2200 kuchukua udhibiti wa mustakabali wao wa kifedha.
Kwa habari zaidi kuhusu QNET na FinGreen, tafadhali tembelea https://www.qnet.net/fingreen/