Filamu mpya ya Tom Cruise, Top Gun: Maverick, imevunja rekodi za filamu. Na wataalamu wa tasnia ya burudani wanamemtaja kuwa nyota namba moja wa filamu duniani.
Lakini, kwa kweli, Tom Cruise hajawahi kuacha kukubaliwa, baada ya kufurahia mafanikio kwa zaidi ya miongo minne!
Amekuwa nyota wa filamu, mwigizaji msaidizi, mtayarishaji, na mkurugenzi, na ameteuliwa na kushinda tuzo nyingi. Cha kushangaza zaidi, nyota huyo, ambaye alifikisha umri wa miaka 60 mnamo tarehe 3 Julai, amefanya yote licha ya ulemavu wa kusoma ambao ulimfanya ashindwe kusoma kipindi chote yuko shule.
Haya hapa ni masomo machache ya maisha kutoka kwa Mr Cruise pekee mwenye kipawa cha kuwatia moyo wamiliki wa biashara na wajasiriamali.
1. Jitoe kwa kila kitu
Cruise amefanya kazi kwa bidii kutoka Siku ya 1. Hakika, imeripotiwa kuwa na shida ya kusoma mistari yake ilimaanisha alipaswa kujituma mara mbili au mara tatu kuliko wenzake ili kufanikiwa..
Ni kweli kwamba siku hizi mambo ni tofauti, kwa kuwa sasa amejifunza kukabiliana na ugonjwa aina ya dyslexia na matatizo mengine. hata hivyo, mwigizaji huyu anabakia kujitolea kufanya kazi kwa bidii.
Kumnukuu Joseph Kosinski, mkurugenzi wa Top Gun: Maverick: “Yeye huipokea kila siku kwa shauku kwamba hiyo ni sinema yake ya kwanza, na wakati huo huo anaweka bidii ndani yake kana kwamba ni sinema yake ya mwisho.”
Mafanikio hayaji kwa urahisi. Hiyo ni wazi kwetu katika uuzaji wa moja kwa moja. Lakini cha muhimu zaidi ni kukumbuka kuwa haijalishi hali yako, uwe ni mgeni au mkongwe, jitoe kwa 110% kila wakati!
2. Usiruhusu chochote kikurudishe nyuma
Hapo zamani, filamu za mapigano (Action) zilitengwa kwa ajili ya waigizaji wenye miaka ya 20 na 30. Lakini si hivyo tena. Na Tom Cruise, zaidi ya wengi, amethibitisha kwamba umri haupaswi kuzuia nafasi za mtu za kufaulu, fursa za kukwea Burj Khalifa na kuruka kutoka kwenye ndege.
Somo hapa, ni rahisi: mafanikio yanaamuliwa na malengo ya mtu, si kwa umri.
Hakika, wajasiriamali wengi walianza safari zao za biashara wakiwa wachanga na wameonja mafanikio. Hata hivyo, kuna wengine wengi ambao wamejiajiri wenyewe baadaye maishani na wakapata utimizo.
Kwa kifupi, unafafanua mafanikio, sio idadi ya mishumaa kwenye keki yako ya mwisho ya kuzaliwa.
3. Tarajia Kukua na kujifunza
Tuweke kando Kazi zake za kustaajabisha, kazi ya Cruise pia inaonyesha kuwa hajawahi kuridhika na kupumzika.
Hakika, gwiji wa filamu anajulikana kwa kujituma kila mara na kujaribu nafasi tofauti – kutoka kuwa mkongwe wa Vita za Vietnam mwenye ulemavu, Aliyezaliwa tarehe Nne ya Julai hadi msimamizi wa Studio mwenye hasira kali katika Tropic Thunder – ambayo inamruhusu kukua kama mwigizaji.
Kujifunza kwa kuendelea na maisha yote ni muhimu kwa ukuaji wa biashara. Na jambo la kuchukua kutoka kwa orodha ndefu ya mafanikio ya Tom Cruise ni kwamba ili kuonja mafanikio ya kweli, wafanyabiashara na wauzaji wa moja kwa moja lazima wawe tayari kutoka nje ya maeneo yao ya starehe, na watazame kujiboresha.
Kuna njia nyingi za kufanya hivyo, bila shaka. Na programu maalum ya kujifunza, kama zile zinazotolewa na qLearn, inaweza kuwa njia nzuri.
4. Jenga imani katika chapa yako ya kibinafsi
Huwezi kumfurahisha kila mtu kila wakati. Lakini tiketi ya maisha marefu katika biashara, kama huko Hollywood, ni uaminifu kwa chapa.
Jina “Tom Cruise” kwenye bango la filamu au tafrija huenda lisihakikishe kuwa watazamaji watapenda filamu. Lakini inachoambia umma ni kwamba nyota huyo amejitoa kikamilifu katika filamu au mradi huo.
Ndiyo maana mashabiki wanaendelea kumiminika kuona filamu zake, lakini pia kwa nini studio hazina shida kupitisha miradi ambayo nyota huyo ameuhusishwa nayo.
Vile vile, katika biashara, kujenga imani ya wateja ni muhimu. Kwa hiyo unafanyaje hivyo? Ni rahisi – timiza ahadi zako, jitolea, shughulikia matatizo papo hapo na moja kwa moja, na kila wakati jitahidi kuwa mtaalamu na mwenye maadili.
Zingatia masomo haya, na wewe, pia, unaweza kuwa na njia ya kazi, yenye mafanikio na yenye kuridhisha.