Katika nyakati hizi za kufutwaa kazi, mfumuko wa bei, na kile ambacho wataalam wanaita “gharama ya maisha”, Jumuiya ya Uuzaji wa Moja kwa Moja Ulimwenguni imeripoti takwimu za ukuaji wa kuvutia katika uchumi wa baada ya janga la uviko, na tasnia hiyo ikiwa na uzoefu wa miaka mitatu. Ikiwa na ukuaji kila mwaka kwa 3.8% kutoka 2018-2021. Ingawa wauzaji wa moja kwa moja ulimwenguni kote wamekuwa wanapitia shida sawa na wato wote duniani, ni muhimu kuzingatia hali ya sasa ya uchumi unapokaribia watarajiwa wapya.
Uchumi Baada ya Janga kuu
Wakati ulimwengu unaendelea kuponataratibu kutokana na athari kubwa za janga hili, watu bado wanajipanga Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limesema mfumuko wa bei mwaka 2022 unaweza kufikia hadi asilimia 5.7 katika nchi zilizoendelea kiuchumi na asilimia 8.7 katika nchi zinazoinukia na zinazoendelea kukua kiuchumi. Mfumuko huu wa kasi wa bei unatoa njia ya kupanda kwa gharama za bidhaa, jambo ambalo humfanya mtumiaji wa kawaida kuwa na wasiwasi zaidi kuliko kawaida kuhusu mahali pesa zao zinatumika. Unaposikia watu wanajiuliza, “Je! ninahitaji hii?” hapo ndipo unapojua ni wakati wa kubadilisha jinsi unavyochukulia uuzaji wa moja kwa moja.
Jinsi ya kufanya Uuzaji wa moja kwa mnamo 2022
Zingatia Matarajio Yako
Ni kawaida kwa wateja wako kuwa na maswali mengi kuhusu QNET, bidhaa zake na uuzaji wa moja kwa moja unahusu nini. Sikiliza hofu na maswali yao, na uwajibu kadri ya uwezo wako. Ikiwa hujui jibu, kuwa mwaminifu na uwaambie utawarudia. Wahimize wafanye utafiti wao wenyewe lakini waelekeze katika mwelekeo sahihi kuhusiana na tovuti na hati rasmi. Kujenga uhusiano mzuri wa kitaaluma na wa uwazi nao utakufaa kwa muda mrefu.
Jieke katika nafasi ya uelewa
Usitupilie mbali wasiwasi wa mteja wako, chochote kile. Jipe muda kusikiliza kwa makini na onyesha kwamba unaelewa hofu zao. Kufanya mauzo sio muhimu kuliko kumfanya mteja wako ahisi kuonekana na kusikilizwa. Hiyo inakuwezesha kuonekana kuwa mtu mwenye ujasiri na anayeaminika, ambayo itaongeza nafasi zako za kuleta mwanachama mpya wa timu.
Fanyia mazoezi mawasilisho yako
Ikiwa huna uhakika na bidhaa na huduma au hata kampuni unapofanya wasilisho lako, tayari umepoteza ofa. Itakusaidia, mbeleni, kujua nini wateja wako watakuuliza na uandae majibu kwa ajili yao. Wateja wako wanahitaji kuhisi kama unawapa thamani, na unaweza kufikia kiwango hicho tu unapofanyia mazoezi mawasilisho yako na kuyakamilisha.
Uza Suluhisho, Sio Bidhaa
Zingatia kwamba watu wanachagua kikamilifu kununua bidhaa zenye ubora wa juu kwa viwango vya juu, wakijua kuwa itawahudumia kwa muda mrefu. Hiyo inakuweka katika nafasi nzuri kama Mwakilishi Huru wa QNET ili kuonyesha sifa za kuboresha maisha kwa bidhaa na huduma za QNET. Weka kama suluhu ya tatizo halisi linalowakabili badala ya kuwa bidhaa tu. Yote yanaposemwa na kufanyika, watajionea wenyewe kwamba bidhaa za QNET pia zimeundwa kudumu, kuthibitishwa kwa kujitegemea na kuzingatia udhibiti wa ubora.
Kuhitimisha
Ni muhimu kufahamu kuwa watu hupatwa na wasiwasi kila wakati. Unapokaribia wateja wapya, kumbuka kwamba watu wanaona vigumu kutumia pesa kwa kitu ambacho hawafikiri ni muhimu. Ni kazi yako kama muuzaji wa moja kwa moja kuwa mvumilivu na kushughulikia wasiwasi wao mwingi kwa njia nzuri na ya kuelimisha iwezekanavyo. Fuata vidokezo hivi na uelekee kwenye uchumi wa sasa na wa baada ya janga hili kwa urahisi.