Kampuni ya biashara ya Mtandaoni Asia yafikia wasiojiweza katika jamii kama sehemu ya maadhimisho ya Ramadhan.
Kama sehemu ya kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, QNET wiki hii ilinyosha mkono wa msaada na kusaidia vituo viwili vya watoto nchini Tanzania. Kwa Bara, mpokeaji alikuwa Mjane Safina na Taasisi ya Huduma ya Watoto, kituo cha watoto yatima huko Kigamboni, Dar es Salaam na kwenye Kisiwa hicho, misaada hiyo ilienda kwa taasisi ya Takrim.